
Mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Ndugu Abbas Ali Mwinyi, ambaye pia ni kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefariki dunia leo akiwa Hospitali ya Lumumba, mjini Unguja leo, Septemba 25.
Marehemu Abbas Ali Mwinyi alijulikana kwa nafasi yake kama msemaji wa familia mara baada ya kifo cha Baba yao, ambapo alisimama mbele ya vyombo vya habari na kueleza msimamo pamoja na taarifa muhimu za kifamilia.
Aidha, kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa mgombea rasmi wa Ubunge wa Jimbo la Fuoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuchaguliwa kuwania tena nafasi hiyo.