Katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani tarehe 29/9/2024 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) itatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Upimaji huu utafanyika bila malipo yoyote kwa watoto na watu wazima tarehe 29/09/2024 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group iliyopo TAZARA wilaya ya Temeke.
Katika kambi hii kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa elimu kuhusu lishe bora na mtindo wa maisha wenye afya ili wananchi wapate uelewa wa kuepuka magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.
Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu ili kama utakutwa na matatizo ya moyo uanze matibabu mapema.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo.