Simba Wanamtaka Kocha Aliyeipeleka Fainali MADAGASCAR Kombe la CHAN
Licha ya makocha wengi kuomba nafasi ya kuifundisha Simba, uongozi wa klabu hiyo upo kwenye mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya MADAGASCAR 🇲🇬 ROMUALD RAKOTONDRABE, aliyeiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya CHAN 2024 iliyofanyika mwaka huu katika nchi za TANZANIA 🇹🇿, KENYA 🇰🇪 na UGANDA🇺🇬.
Chanzo changu cha ndani kimesema “Simba inatafuta kocha haraka ambaye atakuja kabla ya mchezo wa marudiano na kuna uwezekano tukamalizana na kocha wa MADAGASCAR 🇲🇬.
“MOROCCO amekuja kwa ajili ya mechi moja pekee ya marudiano dhidi ya GABORONE UNITED, baada ya hapo timu ndiyo itaendelea kufundishwa na huyo kocha mpya ndiyo maana mchakato unafanyika kwa haraka sana.
“Wakati mchakato ukiendelea na ujio wa MOROCCO, kwa asilimia kubwa MATOLA atakuwa akitoa msaada wa kuijenga timu kwani amekuwa nayo kwa muda mrefu, hivyo hata kama hatokuwa kwenye benchi Jumapili, lakini katika uwanja wa mazoezi atasaidia pakubwa sana.”
Endapo SIMBA SPORTS CLUB itamalizana na Kocha RAKOTONDRABE, basi kibarua chake cha kwanza kinatarajiwa kuwa Oktoba Mosi 2025 dhidi ya Namungo, katika mchezo wa Ligi Kuu utakaofanyika uwanja wa BENJAMIN MKAPA
Julai Mosi 2025, RAKOTONDRABE mwenye umri wa miaka 60, aliteuliwa kukiongoza kikosi cha MADAGASCAR 🇲🇬 kushiriki michuano ya CHAN 2024 na kukifikisha fainali, kikapoteza mbele ya MOROCCO. Kocha huyo mwenye leseni ya UEFA Pro, amekuwa akipenda kutumia mfumo wa 4-3-3…