SELEMAN Matola kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC dhidi ya Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 25 2025.
Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa Simba SC msimu wa 2025/26 kwenye ligi ambayo imeanza kasi Septemba 17 kwa mechi za ushindani kuendelea ndani ya uwanja.
Simba SC imetoka kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Gaborone United ya Botswana inakutana na Fountain Gate ambayo imetoka kupoteza mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0.
Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi cha Simba SC ni Ellie Mpanzu, Kibu Dennis, Moussa Camara, Ladack Chasambi.
Kiujumla Simba na Fountain Gate FC wamekutana mara tatu katika miaka ya karibuni huku Simba ikishinda mechi 2 na mmoja ukiisha kwa sare.
Matola amesema: “Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Fountain Gate ambacho tunahitaji ni matokeo na tunajua kwamba mchezo utakuwa na ushindani mkubwa tupo tayari na wachezaji wapo tayari mashabiki wajitokeze kwa wingi.”