Wananchi mbalimbali wamejitokeza kwenye banda la maonyesho la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika maadhimisho ya siku ya Wahandisi Kitaifa yanayoendelea ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katika Banda la DAWASA wadau wanaojitokeza kupata fursa ya kupata elimu mbalimbali za Mamlaka ikiwemo elimu ya huduma za maji, matumizi ya mita za malipo ya kabla (pre-paid meters), uelewa wa ankara za maji pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto za watumia huduma.
Mamlaka inawakaribisha wananchi wote kufika katika Banda la DAWASA na kupatiwa huduma kwa muda wa siku mbili kuanzia leo 25.9.2025 hadi 26.9.2025