LONDON: MSHAMBULIAJI mpya wa mabingwa watetezi wa EPL Liverpool Alexander Isak anaweza kuanza mechi yake ya kwanza ya Premier League akiwa na Liverpool kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.
Kocha wa Liverpool, Arne Slot amekuwa akimuingiza taratibu mshambuliaji huyo wa Sweden kikosini tangu alipokamilisha usajili ulioweka rekodi ya England ya pauni milioni 125 katika siku ya mwisho ya usajili kwenda Anfield kutokana na kutokuwa na maandalizi mazuri ya kabla ya msimu.
Kufungiwa kwa Hugo Ekitike, aliyepewa kadi nyekundu kwa kuvua shati wakati wa kushangilia bao dhidi ya Southampton Jumanne, kunamaanisha Isak anaweza kuibuka katika kikosi cha kwanza watakapotembelea Selhurst Park.
Fowadi huyo tayari ameanza katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Carabao, ambapo aliifungia klabu hiyo bao lake la kwanza usiku wa Jumanne. Isak bado hajapewa dakika 90 kamili.
Federico Chiesa ni chaguo jingine mbadala wa Ekitike baada ya Muitaliano huyo kuonesha makali yake kwa pasi mbili za mwisho kwenye mchezo dhidi ya Southampton.
The post Isak kuna mchongo anausikilizia first appeared on SpotiLEO.