DAR ES SALAAM:MTAYARISHAJI na mkongwe wa muziki nchini Tanzania, Paul Mattysse maarufu kama P-Funk Majani, ameoneesha uwezo wake mpya kwa kugeukia upande wa tamthilia baada ya kuzindua mfululizo mpya wa maigizo uitwao ‘Mjomba Sele’.
Tamthilia hiyo mpya tayari imeanza kuvutia mashabiki wengi wa filamu na burudani kufuatia uzinduzi wa trailer yake, ikionesha ubunifu mkubwa na mchanganyiko wa mastaa wenye ushawishi mkubwa katika tasnia mbalimbali.
Wanaonekana kushiriki katika tamthilia hiyo ni pamoja na msanii nyota wa muziki Marioo, ambaye pia ni mkwe wa P-Funk Majani, pamoja na muigizaji maarufu Kajala Masanja, ambaye ni mama wa mtoto wa Marioo.
Wengine ni mwanahabari mkongwe Salim Kikeke, rapa mkali Fid Q, muimbaji wa singeli Dulla Makabila, pamoja na waigizaji Ndaro, Steve Mweusi, na Sheikh Abdulrazack, miongoni mwa wengine.
Uwepo wa vipaji kutoka sekta tofauti umeifanya ‘Mjomba Sele’ kuwa tamthilia inayotarajiwa kuleta mapinduzi katika uwanja wa burudani, huku wengi wakitabiri kuwa itakuwa miongoni mwa kazi bora zaidi za mwaka huu.
Kwa mujibu wa Majani, dhamira ya tamthilia hii ni kutoa burudani yenye mafunzo, inayogusa maisha halisi ya kila siku ya Watanzania kwa mtazamo wa kisasa na ubunifu wa hali ya juu.
The post P-Funk Majani azindua tamthilia mpya ‘Mjomba Sele’ first appeared on SpotiLEO.