
Jeshi la Polisi wilaya ya Arusha kwa kushirikiana na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), limetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa, Wakaguzi na Askari kwa ajili ya kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu unaoendelea.
Mafunzo hayo yameyafanyika Septemba 26, 2025 katika bwalo la maafisa wa Polisi Arusha ambapo yamejumuisha Askari kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi akizungumza katika mafunzo hayo amewataka askari kuhakikisha wanatekeleza majukumu kwa nidhamu, kutenda haki, kuwa na weledi na uadilifu.
JE, VIKOBA VYA KAUSHA DAMU NI HARAM? – SHEIKH KANDAUMA AFAFANUA..