
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, limetoa taarifa kuwa watuhumiwa watatu waliokuwa wakituhumiwa kumteka kisha kumuua Shyrose Mabula, mwanafunzi wa Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Mbeya, Shyrose Mahande (21), wameuawa wakati wakijaribu kupambana na polisi wakati wa ukamataji wao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, amewataja waliouawa kuwa ni Marwa Nyahega, Edward Kayuni na Websta Mwantebele.