Kocha Nasreddine Nabi amewasili Jijini Dar es Salaam leo asubuhi, hatua ambayo imezua tetesi kuwa yupo mbioni kutangazwa rasmi kuinoa moja ya timu kubwa nchini.
Kwa sasa haijafahamika ni klabu ipi atajiunga nayo, lakini vyanzo vya karibu vinaeleza kuwa mazungumzo yako katika hatua za mwisho kabla ya kutangazwa rasmi.
Mashabiki wanasubiri kwa hamu kujua ni timu gani itakayofanikiwa kumsajili kocha huyo mwenye rekodi nzuri kwenye soka la Afrika Mashariki.