
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamtafuta Christina Kishiwa, mwenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 40, kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo Sophia Ndoni (3), kisha kutoroka kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea Septemba 29, mwaka huu, katika Mtaa wa Nyakato, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Mashuhuda wanasema kuwa mara baada ya kutekeleza mauaji hayo, Christina aliwaonya ndugu zake kutowataarifu watu kwamba ndiye aliyefanya tukio hilo.
Majirani wa Christina, akiwemo Jenifa Emmanuel na Bakari Hamisi, wameeleza walichoshuhudia. Aidha, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakato, Husein Mwita, ameeleza namna walivyobaini tukio hilo, huku Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Dk. Michael Mushi, akithibitisha kupokea mwili wa marehemu Sophia.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema jeshi la polisi linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa.
Video full ipo YouTube ya Global TV
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
Â