Football ni Mchezo wa wazi,mtu atakwambia uwanja ulikuwa changamoto,ila tujiulize kwenye viwanja vizuri hapa Dar es salaam tumefanikiwa kuiona ile Yanga ya kweli?
Muda mwingine kocha anaweza kujificha kwenye ushindi wa mechi mbili hadi tatu ila kama timu haichezi vizuri ipo siku utaumbuka tu…..siku zote nasema performance nzuri inakupa uhakika wa kushinda mechi ijayo.
Ukweli mchungu ni kwamba Yanga wamesajili vizuri,ila benchi lao la ufundi bado lina mapungufu….hadi Leo Identity ya Folz haijulikani.
Kama huna kocha mzuri ni ngumu Kuona hata ubora wa mchezaji mmoja mmoja.
Yanga wachague kuvumilia au kufanya maamuzi magumu