Klabu ya PSG imethibitisha kuwakosa wachezaji wake wanne kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona siku ya kesho ambao ni Khvicha Kvaratskhelia, Désiré Doué, Marquinhos na Ousmane Dembélé .
Kvaratskhelia alipata jeraha la paja kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Auxerre hivyo ataukosa mchezo huo wakati pia timu hiyo ikiendelea kumkosa mshindi wa Ballon d’Or, Ousmane Dembele, winga Desire Doue na beki wa kati Marquinhos ambao pia wanaendelea kuuguza majeraha yao.