WAKATI tetesi zikieleza kuwa kuna uwezekano wa Roman Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC akakutana na Thank You taarifa zinaeleza kuwa bado yupoyupo ndani ya kikosi hicho.
Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ya NBC msimu wa 2025/26 wamecheza mechi mbili pekee ambazo ni dakika 180.
Mechi ya ufunguzi walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.
Mchezo wa pili walitoshana nguvu kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ukisoma Mbeya City 0-0 Yanga SC.
Ilikuwa ni Desemba 30 2025 walipogawana pointi mojamoja ikiwa ni sare ya kwanza kwa Folz ndani ya ligi msimu wa 2025/26.
Taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa Yaga SC haina mpango wa kuachana na kocha huyo na badala yake wanafanya mazungumzo naye kuona namna ya mwendo wa timu na pale ambapo kunatatizo ili kuboresha zaidi.
Ikumbukwe kwamba kwa sasa watani zao wa jadi Simba SC hawana kocha mkuu hivyo nao wanatajwa kutokuwa tayari kuendelea msimu bla ya kocha.