INAELEZWA kuwa mabosi wa Simba SC wapo na hesabu za kumpa kazi Miguel Gamondi ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Singida Black Stars.
Inaelezwa kuwa Simba SC mara baada ya Fadlu Davids kubwaga manyanga walianza kufikiria kupata huduma ya Gamondi ambaye aliwahi kuinoa Yanga SC na kuipa ubingwa.
Uzoefu wake kwenye soka la Afrika unatajwa kuwa sababu kubwa kwa Simba SC kutuma ofa ndani ya Singida Black Stars kupata saini yake.
Taarifa zinaeleza kuwa uwezekano wa Simba SC kumpata Gamondi ni mdogo kwa sasa kutokana na mpango kazi uliopo kwa mabosi wa Singida Black Stars.
Ushiriki wa Singida Black Stars kwenye anga za kimataifa ikiwa katika Kombe la Shirikisho, uwepo wa wachezaji wenye uzoefu unatajawa kuwa sababu ya Gamondi kutoelekea Simba SC.
Bado mazungumzo yanaendelea na hali itakapofikia hapa tutakujuza msomaji wetu kwa uhakika kuhusu suala la kocha mpya ndani ya kikosi cha Simba SC.