

Mrembo maarufu wa mitandao ya kijamii, Poshy Queen, ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na urembo na muonekano wake (shape), hatimaye amefunguka rasmi kuwa kwa sasa ameolewa na mwanaume anayefanya kazi ya udalali.
Kauli hii ya Poshy Queen imezua gumzo kubwa mitandaoni, hasa ikizingatiwa kuwa awali aliwahi kufunga ndoa na mwanaume kutoka nje ya Tanzania, ingawa ndoa hiyo ilivunjika kutokana na sababu ambazo zilibaki siri yao.
Si hivyo tu, Poshy Queen pia aliwahi kuwa kwenye penzi la mastaa baada ya kutembea na Harmonize, staa wa Bongo Fleva, ingawa uhusiano huo nao uliisha kwa mtafaruku huku mrembo huyo akidai ulikuwa ni penzi la mkataba.
Sasa basi, mnamo Oktoba 1, 2025, Poshy Queen amethibitisha wazi kuwa ameingia kwenye ndoa na Dalali, jambo lililowaacha mashabiki wake wengi wakiwa na mshangao, wengine wakimsifu kwa uamuzi huo huku wengine wakibaki wakijiuliza maswali.
Kwa hatua hii, Poshy Queen anaonesha wazi kwamba maamuzi ya moyo ni yake mwenyewe, na si lazima yaendane na matarajio ya mashabiki au umaarufu aliokuwa nao.
SAKATA la WAKILI wa TUNDU LISSU KUPIGWA MAHAKAMANI – MAWAKILI WAMSHITAKIA IGP WAMBURA kwa JAJI MKUU