Anaandika @kelvinrabson_
✍🏻 Simba walicheza kwenye plan yao ile ile wakiwa na umiliki wa mpira wale mawinga wao wanaingia ndani kwenye “Half Spaces” wakiwa katika mstari mmoja na namba 10 ( Mpanzu , Morice na Mutale ) then fullbacks wanakuwa kama wingers dhumuni wanadumisha mapana ya uwanja wakati wanashambulia …. Faida yake ?
1: Wanakuwa na wachezaji wengi dhidi ya viungo wa chini wa mpinzani na pia wanapata msingi wa mzuri wa kuifungua safu ya ulinzi ya Namungo na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana .
2: Wakati wanaanza build up wanadumisha vizuri overload kwa kuwa na muundo wa 2-2-5-1 , wale CBs wawili wanapata option za kupasia mpira kwa Kagoma na Kante ambao wanashuka chini then Fullbacks wanakuwa pembeni zaidi ya kiwanja ( rahisi kwao kufika eneo la mwisho kirahisi + idadi ya wachezaji wa Namungo wakati wanaweka presha ilikuwa ndogo 2 Vs 4 )
✍🏼 Namungo wamefanya kile kilicho kuwa sawa kwa upande wao , bila mpira wanazuia wakiwa kwenye “Midblock au Lowblock” wanachagua ni nyakati gani watafanya hivo , then wanakuwa karibu karibu sana ( kuweka ugumu kwa Simba kuwafungua ) licha ya kwamba kuna nyakati wanachelewa kwenye matukio hasa nyuma ya mstari wao wa kiungo ambao Simba walikuwa wanatumia vizuri kushambulia . Nafikiri mda mwingine makocha wa hivi vilabu vidogo wanapitia mengi sana kwasababu unaangalia walivyo tengeneza vizuri counter attacks lakini maamuzi ya mwisho hayakuwa sawa ( tatizo linaweza kuwa quality )
NOTE :
1: Simba kwenye “Setpieces” ngumu kukabiliana nao ( wanajua kucheza mipira hiyo 🔥 ) tangia msimu uliopita . Rushine mechi mbili magoli mawili
2: Mutale aliuliza maswali magumu kwenye kiungo cha Namungo ( Sharpness , Dribblers na alifanya vitu vitokee )
3: Namungo kwenye makosa mengi sana kwenye defense yao : Credit kwa Simba wametoa adhabu kwenye makosa hayo .
4: Kisanywa kacheza game nzuri ✅ pamoja na Fabrice naye ( kucheza namba 9 kwa Namungo kwa mechi kama hii ngumu sana )
5: Morice hii nafasi kikosi cha kwanza anaitaka haswa 🔥
6: Mechi mbili , magoli 6 , cleansheets 2
7: Kante passing game 👍🏼
FT: Simba Sc 3-0 Namungo
Uchambuzi By : @kelvinrabson_