
Klabu ya Dodoma Jiji FC imepigwa faini ya jumla ya Shilingi milioni 15 za Kitanzania na Bodi ya Ligi Kuu baada ya kushiriki michezo mitatu bila kuwa na kocha mkuu mwenye sifa stahiki.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, kila timu inatakiwa kuwa na kocha mwenye leseni ya kiwango kinachokubalika na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Hata hivyo, Dodoma Jiji ilionekana kukiuka kanuni hiyo katika michezo yake mitatu iliyopita dhidi ya KMC, TRA United, na Coastal Union.
Kwa kila mchezo, klabu hiyo imepigwa faini ya milioni tano, na kufanya jumla kufikia milioni 15.
Adhabu hiyo imetajwa kama onyo kwa klabu nyingine kuhakikisha zinazingatia matakwa ya kikanuni, hususan katika suala la makocha wenye leseni halali za ukufunzi.
VIJANA ZAIDI 100 WAIPA KAMPUNI ya ULINZI SIKU 7 – UDANGANYIFU WATAJWA – BOSI wa KAMPUNI AKIRI….