Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano na kocha raia wa Bulgaria ๐ง๐ฌ, Dimitar Pantev kuinoa timu hiyo akichukua mikoba ya Fadlu Davids aliyetimkia Raja Casablanca.
Kocha huyo atawasili nchini kesho tar 4 October kwa ajili ya kuanza harakati za kuinoa timu hiyo akitokea Gaborone United ya Botswana ๐ง๐ผ.
Pantev atawasili na msaidizi mmoja kwani makocha wengine waliopo Simba SC bado wapo klabuni ikiwemo Selemani Matola na kocha wa viungo.
Wasifu wa Kocha Dimitar Pantev
Jina kamili: Dimitar Nikolaev Pantev
Tarehe ya kuzaliwa: 26 Juni 1976
Taifa: Bulgaria ๐ง๐ฌ
Leseni ya ukocha: UEFA โA Licenceโ
Mafanikio Makubwa
๐ Ubingwa wa Cameroon (Elite One) msimu wa 2023/24 na Victoria United.
๐ Ubingwa wa Botswana Premier League msimu wa 2024/25 na Gaborone United.
๐ Ameshinda Ligi ya Futsal ya Bulgaria mara tano mfululizo (2011โ2016) akiwa kocha wa Grand Pro Varna.
โย