Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Bi Emma Nyaki (kushoto), akielezea kuhusu matumizi ya nishati mbadala na safi kwa ajili ya kupikia chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Oktoba 6, 2025.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 imeanza kwa shamrashamra nchini huku Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) likipokea pongezi nyingi kwa hatua kubwa ilizozichukua kuboresha huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.
Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya kaulimbiu “Mpango Umewezekana”, yakilenga kuimarisha mawasiliano, uwajibikaji na kasi ya kushughulikia changamoto za wateja kwa wakati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo leo Jumatatu, Oktoba 6, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amesema kuwa TANESCO imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma, hasa kupitia maboresho ya dawati la huduma kwa wateja (Customer Care Desk), hatua iliyopunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.
“Kinachotakiwa ni customer care; huduma bora kwa wateja hujenga imani na uvumilivu. TANESCO imefanikiwa sana katika eneo hilo kwa sasa, mnafanya vizuri sana,” amesema Mtatiro.
“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inapata mrejesho chanya kuhusu huduma zenu, tofauti na awali ambapo malalamiko mengi yalihusu dawati la huduma kwa wateja. Hongereni sana,” ameongeza.
Ameitaka TANESCO kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuwatambua wafanyakazi halali wa shirika hilo ili kudhibiti tatizo la vishoka wanaojitambulisha kwa udanganyifu kama watumishi wa TANESCO.
Aidha, Mtatiro amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, akisema hatua hiyo ni muhimu kwa kulinda mazingira na afya za wananchi.
Kwa upande wake, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amewapongeza wafanyakazi wa TANESCO kwa kujituma na kutoa huduma zenye ubora, huku akihimiza kuongeza kasi zaidi katika kuwahudumia wateja kwa ufanisi na kwa lugha nzuri.
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga
“Tunataka kuhakikisha lengo letu la kuwahudumia wateja wapya 47,192 kutoka 14,990 kwa mwaka huu mkoani Shinyanga linafanikiwa,” amesema Mhandisi Luoga.
“Kitaifa tunalenga kuwafikia wateja wapya milioni 1.7 kutoka 500,000 hapo awali, sambamba na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono juhudi za serikali kulinda mazingira”,ameeleza.
Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Seraphine Lyimo amesema kuwa shirika hilo limejipanga kuendelea kuboresha huduma kwa wateja kwa vitendo kupitia vikao vya kusikiliza maoni ya wananchi, kutoa elimu kuhusu matumizi salama ya umeme, na kuimarisha maadili ya watumishi wake.Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Seraphine Lyimo.
“Tumejipanga kuhakikisha huduma kwa wateja zinaendelea kuimarika zaidi. Tutakuwa tukikutana na wateja mara kwa mara kusikiliza kero na mapendekezo yao ili kuboresha utendaji wetu,” amesema Meneja huyo.
Amesema Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yatatumika kama jukwaa muhimu kwa TANESCO kukutana ana kwa ana na wateja, kujifunza kutoka kwao na kuimarisha uhusiano kati ya shirika na jamii.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kwenye tovuti rasmi ya TANESCO (www.tanesco.co.tz), shirika hilo limekuwa likitekeleza mpango maalum wa Customer Service Improvement Strategy unaolenga kuongeza kasi ya kushughulikia maombi ya wateja, kuimarisha miundombinu ya mawasiliano, na kuongeza vituo vya huduma katika mikoa yote nchini.
Mbali na hilo, TANESCO inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kuongeza upatikanaji wa nishati, ikiwemo Mradi wa Gridi Imara, ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme wa jua (Solar Power Plants) katika mikoa ya Shinyanga na Dodoma, pamoja na kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi majumbani.
Kupitia maboresho haya, TANESCO inaonesha dhamira yake ya dhati ya kutoa huduma bora, za haraka na zenye kuzingatia mahitaji ya wananchi, sambamba na kuunga mkono ajenda ya taifa ya nishati safi na maendeleo endelevu.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Oktoba 6, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Oktoba 6, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Oktoba 6, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Oktoba 6, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Oktoba 6, 2025.Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 ya TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 ya TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 ya TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Seraphine Lyimo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 TANESCO Mkoa wa Shinyanga.Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kulia), akielezea kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati mbadala na safi ya kupikia, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Bi Emma Nyaki (kushoto), akielezea kuhusu matumizi ya nishati mbadala na safi kwa ajili ya kupikia chakula.
Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Bi Emma Nyaki (kushoto), akielezea kuhusu matumizi ya nishati mbadala na safi kwa ajili ya kupikia chakula.
Majiko yanayotumia nishati ya umeme