
Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said, ameteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu vya Wanaume Duniani kwa kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2025 hadi 2029.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, ambaye amesema uteuzi huo ni heshima kubwa si tu kwa klabu ya Yanga, bali pia kwa Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati.
Kwa mujibu wa Kamwe, Eng. Hersi anakuwa mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kati kuteuliwa katika kamati kubwa ya mashindano ya vilabu duniani chini ya FIFA — jambo linaloonesha namna jina la Yanga na Tanzania linavyozidi kung’aa katika ramani ya soka la kimataifa.
KESI YA LISSU BADO KISIKI/SIKU YA PILI BILA TAARIFA ZA POLEPOLE-MAMA AANGUA KILIO/ACT KIKAONI