Hizi takwimu za Madagascar chini ya Romuald Rakotondrabe kwenye CHAN 2024 zinatoa picha ya wazi kuhusu aina ya mpira anaouamini — kocha anayetarajiwa kutuwa Yanga SC, klabu ambayo mashabiki wake wanapenda kuona umiliki mkubwa wa mpira (possession football) na soka la kuvutia.
Uchambuzi by @leomusikula_tz
⚽ 1. Ball Possession – 47.3% mechi saba.
Madagascar haikuwa timu ya kumiliki mpira kwa muda mrefu, bali walitegemea zaidi transitions — yaani kushambulia kwa kasi baada ya kuuteka mpira.
Kocha huyu hakujali sana asilimia ya umiliki, bali ubora wa maamuzi ndani ya sekunde chache.
👉 Kwa Yanga, mashabiki wanatarajia kuona timu ikitawala mpira kwa 60–65%, hasa dhidi ya wapinzani wa ndani. Hivyo, kama Rakotondrabe atatumia mtindo huu wa “compact and reactive football”, kuna hatari mashabiki wakaona timu “haivutii” — japokuwa inaweza kuwa na ufanisi wa matokeo.
🧭 2. Accurate passes – 75% | Own half 84.4% | Opposition half 61.9%
Hapa tunaona falsafa kuu yake:
Anafundisha timu kucheza salama wakiwa nyuma (own half 84.4% accuracy),
Kwa timu kama Yanga ambayo imezoea “build-up play” ya kuvutia kutoka nyuma, hii ni tofauti.
Rakotondrabe anaweza kutengeneza timu inayocheza kwa uelekeo na kasi (direct and quick vertical play) badala ya kupiga pasi 20 kufika langoni.
🧠 3. Long balls (40.6%) na Crosses (24%)
Hii inaonyesha uwepo wa mpira wa moja kwa moja kutoka nyuma kwenda mbele.
Mabeki na viungo wa Madagascar walitumia “long diagonals” kwenda kwa mawinga na washambuliaji na sio mara nyingi kupiga pasi fupi.
📊jumla ya mechi – 7
👉ushindi -4
👉kupoteza- 2
👉sare-1
👉Mabao yakufunga – 9
👉Mabao yakufungwa – 7