Soka la kisasa limebadilika kwa kiasi kikubwa. Siku hizi, mchezo huu hauhitaji matumizi makubwa ya nguvu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, bali unahitaji matumizi makubwa ya **akili** na **ufahamu wa mchezo**.
Ukiangalia jinsi **Ibrahim Bacca** anavyocheza, utaona wazi kuwa bado anaendeshwa na mtazamo wa walinzi wa enzi za miaka ya tisini na kurudi nyuma — enzi ambazo mlinzi alihesabika kuwa bora kwa sababu ya nguvu, ukakamavu, na ukali, bila kuzingatia sana mbinu za kiakili.
Miaka ya nyuma, mlinzi alikuwa anahitajika awe na “akili mbovu,” yaani atumie nguvu zaidi kuliko akili. Lakini leo, mpira umebadilika. Sasa akili ndiyo silaha kuu kwa mchezaji yeyote anayetaka kufanikiwa, hasa katika kiwango cha kimataifa.
Nimekuwa nikimfuatilia Bacca katika michezo mbalimbali, hasa ile ambayo anakutana na washambuliaji wanaotumia akili zaidi kuliko nguvu. Kwenye mechi hizo, Bacca amekuwa akipata changamoto kubwa na mara kadhaa kujikuta akifanya makosa ya msingi — mengine yakiwa na gharama kubwa kwa timu yake.
Kwenye michezo ya kimataifa, ambako anakutana na washambuliaji wenye kasi, uelewa mkubwa wa mchezo, na maamuzi ya haraka, Bacca hujikuta kwenye wakati mgumu. Sababu kuu ni imani yake kwamba **nguvu ndizo kila kitu** katika soka, wakati hali halisi ni tofauti kabisa.
Ni kweli, katika michezo ya ndani (local class), ambapo washambuliaji wengi hawana kasi kubwa ya maamuzi, Bacca anaonekana kama mmoja wa walinzi bora kabisa. Lakini akicheza kwa mtindo huu huu katika kiwango cha kimataifa (**international class**), ni vigumu kwake kufanikiwa.
Matokeo yake yatakuwa:
* Penalti za mara kwa mara,
* Kadi nyekundu,
* Na makosa yanayoigharimu timu.
Ukiangalia penalti ambayo amesababisha jana hakukuwa na haja ya yeye kwenda kutumia nguvu kubwa ya kuucheza mpira na kusababisha penalti
Hapa ndipo tofauti yake na **Dickson Job** inapojitokeza. Dickson anajua kujilinda kwa utulivu, kutumia akili badala ya nguvu, na kuanzisha mashambulizi bila kuhatarisha afya ya mpinzani.
Kwa ujumla, soka la kisasa ni **soka la akili**, si la misuli.