Ameandika Othman Kazi:
“Bacca anatakiwa apate mtu wa saikolojia hayuko sawa. Kuanzia mechi ile na Mbeya City alikuwa ni kama haitaki mechi alifanya makosa mawili makubwa yote ambayo alistahili kadi nyekundu, mbali na tukio la kumkanyaga makusudi Ame Ibrahim, lakini pia dakika ya 33 kaenda kucheza mpira wa juu kwa kumkita goti juu ya bega Matheo Antony ilitakiwa iwe kadi nyekundu, angalia tena alichokifanya mechi akiwa na Taifa Stars, penalty aliyosababisha, kiukweli sio Bacca yule ninayemjua.”
Othman Kazi Mwamuzi Mstaafu.