
…………
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
AFISA Mdhibiti mkuu Ubora wa shule Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Asha Kiliza amesema wazazi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao wanaohitimu elimu ya awali wanaandikishwa mapema kuanza masomo ya darasa la kwanza kwa mwaka 2026.
Amesema wazazi ambao wanawapeleka watoto wao shule binafsi wanatakiwa kuzingatia zile ambazo zimesajiliwa na zinafuata mtaala ulioboreahwa.
Asha ameyasema hayo aliposhiriki mahafali ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya awali katika shule ya msingi ya The Finest iliyopo Kibaha.
Amesema ofisi yake imekuwa ikitoa semina elekezi masuala ya mtaala uliobireshwa kwa shule za binafsi zilizoanzishwa sambamba na kukagua shule hizo kabla hazijapokea wanafunzi.
Kwa mujibu wa Mdhibiti Ubora huyo semina wanayotoa imekuwa ikijikita katika nyanja nane ikiwemo mtaalaunaotumika, vifaa vya mitaala mazingira ya shule pamoja na maadili kwenye shule hizo.
Awali mkurugenzi wa shule hiyo Abubakar Alawi alisema shule hiyo ulianza Octoba 2023 ikiwa na wanafunzi wawili mwalimu mmoja na sasa wamefikia 362 walimu 15.
Mwenyekiti kamati ya shule hiyo ya The Finest Pro. Mrisho Malipula amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa kuwafuatilia wanafunzi na kulipa ada kwa wakati kuepusha kukwama mipango iliyopangwa.
Ameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara hiyo kuondoa changamoto ya magari kuharibika na maeneo mengine kutopitika kipindi cha mvua.