DAR ES SALAAM:Klabu ya Yanga imeamua kuachana rasmi na Kocha wake Mkuu, Romain Folz, aliyekuwa amejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.
Kupitia taarifa iliyotolewa Oktoba 18, 2025 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, Yanga imethibitisha kuwa uamuzi huo umefikiwa kwa makubaliano ya pande zote mbili.
“Uongozi wa Yanga unamshukuru Kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya klabu na unamtakia mafanikio katika majukumu yake mapya,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hizo zinakuja muda mfupi baada ya Yanga kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, matokeo yaliyoongeza presha kwa benchi la ufundi la klabu hiyo.
Hadi anaondoka, Folz alikuwa ameiongoza Yanga kwenye michezo kadhaa ya mashindano ya ndani na kimataifa, lakini matokeo ya hivi karibuni yameonekana kutoridhisha mashabiki na uongozi wa timu hiyo.
The post Yanga mapemaa!, wameona mambo yasiwe mengi first appeared on SpotiLEO.