Baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 ugenini, Kocha mkuu wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi amesema bado ana dakika 90 ngumu za kuandika rekodi ya kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku akiweka wazi bao moja la ugenini ni mtaji mkubwa.
“Haikuwa rahisi licha ya wachezaji wangu kuonyesha mchezo mzuri, makosa machache yametugharimu, tunajipanga kwa mchezo unaofuata tukiwa nyumbani tutaingia kwa kumuheshimu mpishani lakini pia kuhakika tunaandika rekodi mpya.
“Wapinzani wetu ni bora lakini sisi pia ni bora zaidi najivunia wachezaji wangu wote nilionao wana uzoefu licha ya kutanguliwa hawakuonyesha kukubali walipambana na baadae tulipata bao ambalo limetufanya turudi na nguvu.
“Napewa nguvu na wachezaji wangu wana utayari wa kufikia malengo na wamenihakikishia kuwa tuna nafasi ya kufuzu hatua inayofuata, hivyo kazi yangu ni kusuka mipango mikakati imara, utayari wa wachezaji ndio itakuwa chachu yetu,” alisema Gamondi.