Leo ni Siku nyingine ya kuwakumbusha umuhimu wa kumshirikisha Kocha kwenye usajili
Simba SC ya Meneja Pantev , ndio Simba hii hii ambayo kwa majuma kadhaa nyuma ilikuwa chini ya Matola na Morocco baada ya kuondoka kwa Fadlu
Ukikusanya maoni ya wadau leo Jumanne watu watakwambia hii Simba ni timu haswa kwa sababu wamependa walichokiona Jumapili na siku kadhaa nyuma.
Kwa upande wangu hii Simba siipimi kwa matokeo ya dakika 90 , wala siangalii uchezaji wa timu kwa hizi siku kadhaa ili niseme bora.
Nimeangalia talent ya kuzaliwa nayo kwa mchezaji mmoja mmoja , kujitoa wakiwa uwanjani na uwezo wa kutafsiri kile anachoelekezwa na mwalimu , hapo sasa nikasema Simba SC timu wanayo.
Bila hiyana ndio kwanza mzunguko wa 2 Ligi kuu na hatua ya awali CAF CL haya maua nayarudisha kwa kocha Abdulrahman Fadlu ambaye kwa zaidi ya 70% yeye ndiye aliyefanya huu usajili
Hizi mashine zote yeye ndiye alisema nileteeni zinifanyie kazi yangu , kuona kwamba hakubahatisha Fadlu ameondoka lakini wanajeshi wake wanaendelea kuonesha hawakuja Simba kwa kubebwa bali uwezo.