

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeuzuia rasmi wimbo wa msanii Ibrahim Mussa, maarufu kama Roma Mkatoliki, unaoitwa “Teremsha Bunduki”, hadi utakapofanyiwa marekebisho.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya BASATA, wimbo huo ulitolewa tarehe 10 Oktoba 2025 chini ya lebo za Kitonzomadeit na SMG Family. Hata hivyo, baraza hilo limeupa wimbo huo daraja la KK (R), likimaanisha kuwa haukidhi vigezo vya kuonyeshwa au kupigwa hadharani katika maeneo yoyote nchini.
BASATA imeeleza kuwa, licha ya wimbo huo kutokuwa na upotoshaji, uongo au uchochezi, umebainika kukosa ulinganifu na Kanuni ya 25(6)(b) ya mwaka 2018, hivyo kuhitaji marekebisho kabla ya kuruhusiwa kusambazwa.
Aidha, baraza hilo limepiga marufuku wimbo huo kuchezwa katika vyombo vya habari au mitandao ya kijamii hadi utakaporekebishwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
BASATA imeonya kuwa mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa Kanuni ya BASATA ya mwaka 2018, kifungu cha 25(8)(a) na (b).
VIDEO INAYOTREND ya MAMA AKIPIGWA VIBAO na MWENZAKE ENEO la BIASHARA – WAZIRI GWAJIMA ANAMTAFUTA….