KUTOKA KIJIWENI
Kwa mwenendo wake performance za wachezaji wapya wa Yanga ni wazi ya kwamba Kocha Romain Folz alikaribia kuwachoresha na kuwachongea viongozi wa Yanga kwa mashabiki na wanachama wao ya kuwa wachezaji waliowasajili wengi ni magarasa.
Ikumbukwe Rais wa Yanga,Injinia Hersi Said alinukuliwa akisema pengine huu ndio usajili wake bora kuwahi kuufanya tangu aingia klabuni hapo .
Kauli hii ya Injinia Hersi Said inakinzana pakubwa na kinacho onekana uwanjani jambo ambalo kiuhalisia kama viongozi lazima wajiulize mara mbili,je Célestin Ecua ,Balla Conte,Lassine Kouma, Zimbwe Jr ni wachezaji wa kawaida?wakaamua wamtimue Romain Folz.
Swali ni je,Kocha ajaye atafanikiwa kuwafichia aibu viongozi wa Yanga kwenye hili?