
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza rasmi vikwazo vipya dhidi ya baadhi ya makampuni makubwa ya mafuta kutoka Urusi, hatua inayolenga kuongeza shinikizo kwa serikali ya Rais Vladimir Putin kufuatia kuendelea kwa mvutano wa kisiasa.
Vikwazo hivyo vinahusisha kufungia mali za makampuni kadhaa na kuzuia biashara ya mafuta kati ya Urusi na washirika wake wa kimataifa.
Hatua hiyo imesabisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani, huku wachambuzi wakionya kuwa inaweza kuongeza gharama za nishati katika nchi nyingi.
Serikali ya Urusi imelaani hatua hiyo, ikidai kuwa Marekani inajaribu kutumia nguvu za kiuchumi kama silaha ya kisiasa.
Hata hivyo, Ikulu ya Marekani imesisitiza kuwa vikwazo hivyo ni sehemu ya juhudi za kulinda maslahi ya kimataifa na kudhibiti ufadhili wa kijeshi wa Urusi.