Wasimamizi wa mashamba ya parachichi kutoka mikoa ya Njombe ,Ruvuma ,Mbeya na Iringa wamekutanishwa mjini Njombe na kampuni iliyojipambanua katika kuinua sekta ya kilimo Guavay ltd na kisha kuwapa mafunzo ya kujengewa uwezo wa matumizi bora ya mbolea,viuatilifu ,udhibiti na usimamizi mzuri wa mashamba pamoja na afya ya udongo ili kumfanya mkulima kufanya kilimo chenye tija kinachokidhi hitaji la soko la kimataifa.
Awali Azalia William ambae ni afisa masoko na mauzo kampuni ya Guavey mzalishaji wa mbolea za hakika akieleza sababu ya kutoa mafunzo hayo amesema ni kwasababu wakulima wengi wamekuwa wakitumia mbolea kinyume cha utaratibu na kwamba kunzia sasa mkulima watajua afya za udongo uliyopo kwenye shamba yao namna ya kutibu ili kupata mazao ya kutosha katika uwekezaji wao.
William amesema endapo wakulima watafanya kilimo bora na chenye tija watainua kipato chao na kunguza mazao yasio na sifa sokoni na kwamba ili kufikia lengo hilo kampuni inatoa pia huduma za ugani na elimu mara kwa mara kwa wakulima.
Akitoa ujumbe wa serikali wakati akifungua mafunzo hayo afisa kilimo mkoa wa Njombe Wilson Joel amesema ya takuwa na matokeo chanya kwa wakulima kwakuwa wengi wao walikuwa hawajui namna sahihi ya kutumia mbolea hususani kwa kiasi gani,wakati gani na sehemu gani ili kupata mavuno yanayo stahili huku akiyataka wadau wengine kuendelea kutoa elimu kwa wakulima.
Aidha Joel amesema kitendo cha kuwapa elimu niyo wasimamizi wa mashamba ya parachihi kinaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali za kuzunguka katika mikoa yote nchini kutoa elimu ya matumizi bora ya mbolea na kisha kuwahimiza washiriki kuzingatia ili wakachane na kilimo cha mazoea.
Kwa upande wanufaika wa mafunzo hayo akiwemo Eligius Wella maarufu madebe ambae ni muwekezaji na msimamizi wa mashamba ya parachichi mkoani Njombe wamesema ,imewafungua macho kwasababu wengi walijikita katika matumizi ya mbolea za samadi bila kujua inaukosefu wa virutubisho vingine hivyo kuanzia sasa watakuwa wakitumia na mbolea zanye virutubisho vingine kama vile mbolea za hakika huku wengine wakiomba idadi ya maafisa ugani kuongezwa ili wakasaidie wakulima.
Washiriki wa mafunzo hayo wametoka mikoa ya Iringa,Ruvuma,Mbeya na Njombe.