

Mwigizaji wa filamu, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mwanaharakati, Lulu Mapunda, ambaye awali alikuwa akihamasisha maandamano Oktoba 29, amesema sasa haoni sababu ya kuandamana, akisisitiza umuhimu wa kuruhusu uchaguzi ufanyike kwa amani ili kila mmoja atumie haki yake ya kikatiba.
Ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati akizungumza na wanahabari, akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo na demokrasia.
“Ni vizuri kuwaruhusu Watanzania kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi bila vuguvugu lolote la uvunjifu wa amani. Wanaharakati waliopo nje ya nchi njooni nyumbani, tuungane pamoja baada ya uchaguzi,” amesema Lulu.









