“Hii inaweza kuwa taarifa mbaya kwa mashabiki wa Yanga, baada ya mshambuliaji wa kikosi hicho, Clement Mzize, juzi kujitonesha jeraha la goti na huenda akafanyiwa upasuaji ili kumtibu”
“Taarifa kutoka kambi ya Yanga, zililiambia Arena TV kuwa, Mzize amewatia hofu tena kwani juzi jioni katika mazoezi ya mwisho kuelekea kuikabili Silver Strikers, alijitonesha jeraha lake la goti ambalo awali ilielezwa amepona”
“Kuna uwezekano akafanyiwa upasuaji wa goti nje ya nchi, hivyo kumpata kwenye mechi za karibuni ni bahati sana,” kilisema chanzo








