Kwa mara ya kwanza kwenye historia, Ligi kuu soka Tanzania imeingiza timu 4 kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu.
Timu za Tanzania zilizofuzu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ni Simba SC na Yanga SC.
Timu za Tanzania zilizofuzu kwenye Kombe la shirikisho Afrika msimu huu ni Azam FC na Singida Black Stars FC.




