Klabu ya Yanga imetangaza kutumia Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kwenye mechi tatu za nyumbani katika hatua ya makundi, michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
“Yanga imesema uamuzi huo umezingatia maslahi mapana ya klabu.
Tumeshawasiliana na wenzetu wa Zanzibar na tumekubaliana kwenda huko. Hizi ni mechi ngumu na zinahitaji maandalizi yenye utulivu. Tungebaki hapa Dar, tunajua kuna uwezekano mkubwa tukakutana na mazingira ya kukwamishana na hatutaki tukutane,”
Tumetafakari kwa kina na kutokana na mechi hizo za kundi tulilopo kuonekana kuwa ngumu tunahitaji kujipanga vizuri na kwa masilahi mapana ya Yanga mechi zetu tatu za makundi zitapigwa visiwani Zanzibar” Yanga
The post Yanga Waikimbia Simba Kwa Mkapa Waogopa Figisu Ligi ya Mabingwa CAF appeared first on Soka Tanzania.



