NEWYORK: WAPENZI maarufu wa muziki wa Marekani, Big Sean na Jhené Aiko, wanadaiwa kuvunjika kwa uhusiano wao baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya muongo mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa za jarida la burudani AllHipHop, vyanzo vya karibu na wawili hao vimeeleza kuwa uamuzi wa kuachana umetokana na kutokubaliana kuhusu mustakabali wa uhusiano wao.
Chanzo hicho kilidai kuwa Aiko alitaka kujitolea zaidi kwenye ndoa, huku Big Sean akionekana kusita kuchukua hatua hiyo kubwa.
“Alitaka ndoa, alitaka kujua amejitolea kwa dhati,” kilisema chanzo hicho.
“Sean anampenda sana, lakini hakuwahi kuwa tayari kuchukua hatua hiyo ya mwisho.”
Inadaiwa kuwa kabla ya kuondoka, Aiko alimpa Big Sean masharti kadhaa ya mwisho lakini mwishowe alitambua kuwa hakukuwa na mpango wa pete ya uchumba.
“Wako kwenye hali nzuri kwa amani,” chanzo hicho kiliongeza. “Wana heshimiana mno kiasi cha kutotaka mambo yawe machafu. Kila mmoja anataka kilicho bora kwa mtoto wao.”
Hadi sasa, hakuna kati ya wasanii hao aliyetoa kauli rasmi kuhusu hilo.
The post Big Sean na Jhené Aiko wavunja uhusiano baada ya miaka 10 first appeared on SpotiLEO.



