DAR ES SALAAM: BAADA ya maneno makali ya bondia wa Kenya Rayton Okwiri kwamba Hassan Mwakinyo anamkwepa hataki kupambana naye , Mwakinyo hakuacha jibu lipite.
Kupitia ujumbe aliouweka mtandaoni, Mwakinyo amefichua kuwa tayari kulikuwa na mazungumzo ya pambano, na akaonesha ‘screenshot’ za tarehe na mawasiliano kuonesha kuwa hakuwa mkimbiaji kama anavyodaiwa.

“Kwa mujibu wa mmoja wa watu waliomtafuta nicheze naye, haya ndiyo yalikuwa majibu yake. Utaona tarehe na mwezi,” ameandika Mwakinyo.
Maelezo aliyoweka Mwakinyo yanaonesha wazi Okwiri ndiye aliyemkimbia.
“Mimi sina neno jingine la ziada. Saini mkataba nikuonyeshe kuwa nguo za jeshi wakati mwingine huvaliwa na maharusi. Ambieni huyo karau.”
The post Mwakinyo amuita Okwiri wamalize ubishi first appeared on SpotiLEO.






