RIYADH: MSHAMBULIAJI wa Al Nassr na Twiga Stars Clara Luvanga, ameendeleza moto wake katika Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia baada ya usiku wa jana kufunga hat-trick na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Neom.
Katika mchezo huo uliochezwa mjini Riyadh, Luvanga alionesha ubora wake wa kawaida kwa kutumia kasi, nguvu na umaliziaji makini ambao umeendelea kumfanya kuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi kwenye ligi hiyo msimu huu.
Ushindi huo umeiwezesha Al Nassr kuendelea kusogea kileleni mwa msimamo huku mkononi wakiwa na mshambuliaji ambaye anaendelea kuweka rekodi nyingine muhimu katika msimu wake wa pili nchini humo.
Kwa hat-trick hiyo, rasmi Luvanga ameifikisha jumla ya mabao 11 katika mechi sita alizocheza msimu huu, na kuendelea kukalia usalama wa nafasi ya kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia.
Luvanga, ambaye ameendelea kuwa sura muhimu kwenye kikosi cha Twiga Stars, ameongeza sababu nyingine kwa Watanzania kuendelea kumfuatilia kutokana na kasi yake ya kipekee inayomfanya kutamba katika soka la wanawake barani Asia.
The post Luvanga azidi kuweka rekodi Saudi Arabia first appeared on SpotiLEO.






