Habari njema imewajia mashabiki wa klabu ya Young Africans kufuatia kuonekana kwa kiungo wao mahiri Clement Mzinze akifanya mazoezi mepesi baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha.
Kuonekana kwake uwanjani kumezua matumaini makubwa na ishara kwamba furaha ya wananchi huenda ikarejea mapema zaidi ya ilivyotarajiwa.
Mzinze, ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo na anayependwa sana na mashabiki kutokana na kiwango chake cha juu cha kukaba na kuanzisha mashambulizi, alikumbana na jeraha baya ambalo lilimlazimu kukaa kando ya uwanja akipokea matibabu.
Kutokuwepo kwake kumeonekana kuacha pengo kubwa kwenye safu ya kiungo ya Yanga katika baadhi ya michezo muhimu.
Katika kambi ya mazoezi ya Yanga, Mzinze alionekana akifanya mazoezi ya viungo vya mwili na kukimbia kwa taratibu, huku akisimamiwa na wataalamu wa tiba ya viungo wa timu hiyo.
Ingawa bado hajajiunga na mazoezi kamili ya timu, hatua hii inatajwa kuwa ya maendeleo makubwa katika kurejea kwake.
Kumuona Clement akifanya mazoezi ni faraja kubwa tunamhitaji sana kwenye timu, ubora wake wa kupambana kiungo unakosekana alisema mmoja wa mashabiki wa Yanga aliyekuwa akifuatilia taarifa hiyo kwa karibu.
Wataalamu wa afya wameeleza kuwa Mzinze anaendelea vyema na huenda akarejea uwanjani rasmi kuanza kuichezea timu hiyo katika kipindi kifupi kijacho.
Kurudi kwake kutampa kocha chaguo zaidi la wachezaji na kuongeza ushindani katika safu ya kiungo, jambo litakaloongeza ubora wa timu.
Kurejea kwa Mzinze kunaashiria mwisho wa siku ngumu kwa mashabiki, ambao walikuwa na wasiwasi kuhusu hali yake.
Sasa, macho yote yameelekezwa kwenye tarehe ya kurejea kwake kamili huku wakiota mafanikio makubwa atakayoleta uwanjani.
The post Habari Njema Kwa Yanga, Clement Mzize Aonekana Akifanya Mazoezi appeared first on SOKA TANZANIA.



