Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na Mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappé ameondoka kwenye kambi ya Timu ya Taifa na kurejea kwenye klabu yake kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi ya jeraha lake.
Mbappe licha ya kucheza mchezo wa jana dhidi ya Ukraine na kuandika historia ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kwa karne ya 21 kufunga magoli 400 katika michezo 537 bado anasumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu wake wa kulia.
Mshambuliaji huyo ni rasmi ataukosa mchezo unaofuata wa Nchi yake dhidi ya timu ya Taifa ya Azerbaijan siku ya Jumapili.



