LOS ANGELES: MKE wa aliyekua muigizaji wa Black Panther Chadwick Boseman, Simone Boseman amesema Chadwick alikua na moyo wa ajabu sana kiasi kwamba angeweza kutoa nafsi yake kwa yeyote.
Simone ameeleza hayo alivyokua akipokea tuzo ya ‘Walk of Fame’ ambayo ametunukiwa Chadwick Boseman ambaye ni mume wake.
“Chadwick alitufundisha wote mambo mengi sana, moyo wake ulikua mpana sana kiasi kwamba angeweza kumpa kila mtu sehemu yake maalum na bado angekuwa na mengi ya kushiriki na ulimwengu” Simone alisema.
Hata hivyo Simone alisema richa ya mume wake kufariki bado anahisi uwepo wake kila siku.
Katika tukio hilo Simone aliongozana na wasanii mbalimbali wa Black Panther akiwemo Michael B Jordan na Letitia Wright pamoja na mtayarishaji Ryan Coogler.
The post Mjane Simone Boseman aleta kitu cha thamani ‘Walk of Fame’ first appeared on SpotiLEO.





