NAPLES: BEKI wa Qarabağ Kevin Medina aliyezimia baada ya kupigwa na shuti kali la mchezaji wa Napoli Scott McTominay katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumanne anaendelea vizuri.
Medina alianguka chini dakika ya 51 baada ya mpira kumpiga usoni kwa nguvu kutoka karibu, na mcolombia huyo alionekana kutotikisika akiwa hapo chini kwa karibu dakika moja.
Timu ya madaktari ilikimbia uwanjani mara moja, pamoja na gari maalum la kumtoa mchezaji, lakini Medina alisisitiza kuendelea na mchezo na akaweza kurejea baada ya uchunguzi wa haraka wa mtikisiko wa ubongo.
Hata hivyo, aliendelea kuonekana kupepesuka na kulazimika kutolewa nje dakika 10 baadaye. Mapema leo madaktari wa klabu hiyo wamesema beki huyo hakupata majeraha makubwa na anaendelea vizuri.

The post Aliyezimia uwanjani aendelea vizuri first appeared on SpotiLEO.









