LONDON: Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane, alikuwa na siku mbaya kazini wakati miamba hiyo ya Ujerumani ikipokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Arsenal kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano ikiwa ni kipigo chao cha kwanza msimu huu.
Nahodha huyo wa England, ambaye tayari amefunga mabao 29 kwenye mashindano yote msimu huu kwa klabu na timu ya taifa, amesema hakuna sababu ya kutaharuki, akitabiri kuwa huenda timu hizo zikakutana tena hatua za juu za mashindano au msimu ujao wa masika.
“Ilikuwa mechi ngumu kama tulivyotarajia. Tulipambana vizuri kipindi cha kwanza, kilikuwa sawa kwa kiasi Fulani. Kipindi cha pili hatukuwa na nguvu na kasi ile ile, na tulipoteza duels nyingi.”

“Hiki ndicho kipigo chetu cha kwanza msimu huu. Hatutaki kuwa na hofu kupita kiasi kuhusu hilo, lakini bila shaka tutajifunza. Nina hakika tutakutana tena (Arsenal) kwenye hatua za juu za Ligi ya Mabingwa.” – amesema Kane
Akiwa Tottenham, Kane alifunga mabao 14 katika mechi 17 za North London derby kwenye Premier League. Pia alifunga penalti dhidi ya Arsenal kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa misimu miwili iliyopita, ambapo Bayern walishinda jumla ya 3-2.
Lakini Arsenal sasa wamekua na kuimarika zaidi, wakinufaika na matumizi makubwa ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililoongeza kina na upana wa kikosi ambacho hata Bayern hawawezi kujilinganisha nacho.
The post Kane ataka utulivu Bayern first appeared on SpotiLEO.





