
Pamoja na Simba kupoteza mchezo wa jana ambao ni mchezo wa pili mfululizo kwa hatua ya makundi , Meneja Dimitar Pantev amejitahidi sana kiuchezaji kwa kulinganisha na mchezo wa kwanza ambao mimi pia ni katoka waliomkosoa .
Nimejiridhisha kuwa Simba SC ndio timu iliyotengeneza nafasi nyingi zaidi kwa siku ya jana kwenye mechi zote za CAF [ CL & CC ]
Simba alikuwa na uwezo wa kupata mabao hadi 5 kama nafasi zote zingetumika ipasavyo
[ Ahoua , Mutale , Mutale , Mukwala + Maema ] nilizozisahau utaongeza hapo.
Kwenye mashindano ya CAF kupata nafasi za wazi ni jambo gumu sana ndio maaana mabao yanakuwa machache , lakini Simba ni timu iliyofanikiwa sana kwenye hilo , wana mwalimu ambaye tutamuhukumu kama timu haitengenezi nafasi lakini suala la kumalizia nafasi ni mchezaji binafsi na sio mwalimu.
Kama nilivyotoa lawama kwa mwalimu mechi ya kwanza , leo natoa pongezi kwa kubadilisha kitu kikosini japo wamekosa matokeo
The post Shaffih Dauda “Tusimlaumu Kocha wa Simba Pantev Kufungwa Kwa Simba” appeared first on SOKA TANZANIA.


