BRIGHTON: KOCHA wa Everton, David Moyes, amemtetea winga Jack Grealish akisema hajawa hasara tangu ajiunge na klabu hiyo kwa mkopo kutoka Manchester City, licha ya ukosoaji unaofuatia kupungua kwa kiwango chake siku za hivi karibuni kabla ya kufunga bao lake la pili msimu huu katika ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Bournemouth, Jumanne.
Grealish, mwenye miaka 30, alianza kwa kiwango cha juu katika mechi zake za mwanzo baada ya kuwasili Goodison Park Agosti, lakini alikumbwa na kushuka kiwango, akifunga bao moja tu katika mechi 14 kabla ya kufumania nyavu tena dhidi ya Bournemouth hapo jana.
Bao lake lilikuja dakika ya 78 kwa shuti lililogonga mchezaji wa Bournemouth, Bafode Diakite, hali iliyomfanya Moyes kucheka akisema huenda lingehesabiwa kama bao la kujifunga.

“Kikubwa kwa Jack kwa sasa ni kupata muda mwingi wa kucheza. Anatuonesha kiwango kizuri kwa kutoa assist au kufunga. Amecheza mechi kadhaa ambapo angeweza kuwa bora zaidi, lakini bila shaka anatupa kitu.” – amesema Moyes
Moyes pia alisema mashabiki wa Everton wamekuwa wakimkubali Grealish kutokana na tabia na namna yake ya kujituma uwanjani.
“Ninataka afunge mabao zaidi. Nimekuwa nikimwambia: ‘Assist zako ni nzuri, lakini nahitaji mabao zaidi.’ Ni mchezaji muhimu kwetu na anatusaidia kuendelea kuwa bora,” – ameongeza
Grealish, bingwa wa Premier League na Champions League akiwa Manchester City, alipoteza nafasi yake Etihad kutokana na majeraha na taarifa za maisha yake ya starehe nje ya uwanja.
Hata hivyo, akiwa Everton, amesema anafurahia muda wakeklabuni hapo, akisema uhusiano wake mzuri na Kocha Moyes umechangia kumrudisha kwenye kiwango nzuri.
The post Moyes amkingia kifua Grealish first appeared on SpotiLEO.





