Kiungo wa Young Africans, Maxi Nzengeli, amefunguka kuhusu timu anayoitamani zaidi barani Afrika, akieleza wazi kuwa moja ya ndoto zake ni kuwahi kuchezea mabingwa wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.
Maxi ameeleza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na ubora wa soka linalochezwa na Mamelodi, pamoja na namna klabu hiyo inavyoendeshwa kitaalamu na kisasa, jambo ambalo linaifanya kuwa moja ya timu bora zaidi barani Afrika.
Amesema mfumo wa uchezaji, nidhamu ya kikosi na namna ambavyo wachezaji huendelezwa ndani ya klabu hiyo ni mambo yaliyomfanya aipende Mamelodi na kuona ni mahali sahihi kwa mchezaji anayetamani kupiga hatua kubwa katika soka la kulipwa.
Hata hivyo, Maxi amebainisha kuwa kwa sasa anajikita katika kuisaidia Yanga katika michuano ya ndani na ya kimataifa, huku akiamini kuwa ndoto zake zinaweza kutimia kupitia juhudi na kiwango anachokionesha.
The post Maxi Nzengeli “Ndoto Zangu ni Kucheza Mamelodi” appeared first on SOKA TANZANIA.








