WAKATI Rais wa Yanga, Hersi Said, akiwa ametia saini makubaliano na wakala Zambro Traore kuhusu uwezekano wa kuleta wachezaji wapya, kocha mkuu wa timu hiyo Pedro Gocalves amethibitisha kuwa dirisha dogo litakapofunguliwa atalenga kufanya maboresho muhimu ndani ya kikosi chake.
Mazungumzo hayo yamekuja katika kipindi ambacho Yanga inajiandaa kwa mikikimikiki ya michuano ya ndani na ya kimataifa.
Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Januari, unakusudia kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimeonyesha ubora msimu huu, lakini bado kinahitaji uimarishaji ili kuhimili ushindani mkubwa unaowakabili katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza kuhusu mipango yake, Pedro amesema licha ya kuwa na kikosi kizuri, bado anaona kuna maeneo yanayohitaji kuongezewa ubora.
Amedai kuwa ni muhimu kuongeza wachezaji wenye uwezo wa kuongeza ushindani ndani ya timu, kuhakikisha wanaendelea kuwa bora zaidi ya walivyokuwa msimu uliopita.
“Tutaangalia na kuona nini tunaweza kufanya. Tunahitaji maboresho madogo kwa lengo la kuimarisha kikosi katika maeneo yenye mapungufu,” alisema Pedro. ameonyesh dhamira ya kuboresha bila kuvuruga mfumo uliopo.
Kocha huyo ameonekana kutaka wachezaji watakaoongeza chachu na kuleta ushindani wa moja kwa moja ndani ya kikosi.
Kwa upande mwingine, wakala Zambro Traore, ambaye amekuwa na wachezaji kadhaa wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara akiwemo Pacome Zouzoua, Charles Ahoua, Karaboue Chamou na Yao Antony Trabi, amefunguka kuhusu ziara yake jijini Dar es Salaam. Amesema mbali na kuwatembelea wachezaji wake, pia alikuwa kwenye mazungumzo na Rais wa Yanga anadhani dirisha Dogo kutakuwa na ongezeko la wachezaji.
The post HERSI AKUTANA NA WAKALA WA WACHEZAJI, PEDRO ATAKA appeared first on Soka La Bongo.






