BODI ya Wakurugenzi ya klabu imekutana katika kikao muhimu kilichoongozwa na Mwenyekiti wake, Crescentius Magori, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa klabu hiyo katika kipindi hiki cha ushindani.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe wa bodi pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa klabu, ambapo kililenga kufanya tathmini ya mwenendo wa timu katika mashindano yanayoendelea na kuweka mikakati ya kuboresha matokeo siku zijazo.
Moja ya ajenda nzito zilizojadiliwa ni suala la Kocha Mkuu, ambapo bodi ilipitia kwa kina ripoti ya kiufundi kuhusu utendaji wa benchi la ufundi na mwelekeo wa timu kwa ujumla, ili kuhakikisha malengo ya klabu yanaendelea kutekelezwa ipasavyo.
Aidha, bodi ilijadili kwa kina dirisha dogo la usajili, ikitathmini maeneo ambayo timu inahitaji kuimarishwa pamoja na uwezekano wa kuingia sokoni kusaka wachezaji watakaoongeza ushindani na ubora ndani ya kikosi.
Katika majadiliano hayo, ilisisitizwa kuwa maamuzi yatakayochukuliwa yatazingatia maslahi mapana ya klabu kwa muda mfupi na mrefu, huku nidhamu, ubora na dira ya maendeleo ikiendelea kuwa msingi wa maamuzi yote.
The post BODI YA WAKURUGENZI YAJADILI HATMA YA KOCHA appeared first on Soka La Bongo.








