KLABU ya Simba imemtangaza rasmi kocha mkuu mpya, Steve Berker, ambaye anachukua nafasi ya Dimitar Pantev aliyekuwa akiiongoza timu hiyo kwa nafasi ya Meneja.
Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya kiufundi yanayolenga kuimarisha kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kuelekea michuano iliyopo mbele yao.
Berker anatarajiwa kuanza kazi rasmi Desemba 28, 2025, mara baada ya timu kurejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa. Uongozi wa Simba unaamini ujio wake utaongeza ushindani, nidhamu na ubora wa kikosi.
Kocha huyo ana uzoefu mkubwa katika soka la Afrika, akiwa ametokea Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, klabu inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu. Msimu uliopita, Stellenbosch FC iliwahi kukutana na Simba katika michuano hiyo, jambo linaloonyesha kuwa Berker anaifahamu vizuri timu hiyo na ushindani wa soka la Afrika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, amesema kuwa pamoja na kumpa jukumu la kuinoa timu, Berker pia amekabidhiwa dhamana ya kusimamia mwelekeo wa usajili katika dirisha dogo lijalo. Hatua hiyo itazingatia ripoti ya benchi la ufundi pamoja na tathmini ya kocha mkuu.
Magori ameeleza kuwa uongozi ulilazimika kusubiri kwanza kocha mpya kufanya tathmini ya kina ya kikosi kilichopo kabla ya kufanya maamuzi yoyote kuhusu kuongeza au kuwaondoa baadhi ya wachezaji, ikiwemo kuwapeleka kwa mkopo.
Amefafanua kuwa mchakato wa usajili hautafanywa kwa pupa, bali utaongozwa na mahitaji halisi ya timu kulingana na tathmini
The post SIMBA YATANGAZA KOCHA MPYA, MAJUKUMU MAZITO NA appeared first on Soka La Bongo.







